Kamisheni ya UM ya maendeleo endelevu yapiga hatua

Kamisheni ya UM ya maendeleo endelevu yapiga hatua

Wajumbe wa kamishna ya umoja wa mataifa wanaohusika na mpango wa maendeleo endelevu wamepiga hatua kubwa kufikia shabaya iliyokusudiwa jambo ambalo linatia matumaini makubwa kwa siku za usoni.

Kulingana na Mwenyekiti wa kamati hiyo László Borbély wajumbe hao wameweza kuzingatia maeneo kadhaa ikiwemo yale yanayohusu madini, usafiri na usimamizi wa taka.

Hata hivyo amesema kuwa pamoja na kuendelea na mchakato ambao baadaye utatoa sura ya makubaliano yatakayohusu nchi kwa pamoja lakini hata hivyo baadhi ya nchi bado zinaendelea kusua sua kufikia shabaya hiyo.

Kasoro hizo zinatarajiwa kujadiliwa kwenye mkutano mkuu ujao wa mazingira ambao umepangwa kufanyika mwaka ujao wakati ambapo mawaziri kutoka nchi zaidi ya 50 wanapokutana kujadilia masuala mbalimbali.