Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka operesheni za kijeshi Libya zisitishwe

UM wataka operesheni za kijeshi Libya zisitishwe

Maafisa wa kutoa misaada wa umoja wa mataifa wametaka kusitishwa kwa muda operesheni za kijeshi nchini Libya ili kupisha shughuli za utoaji misaada ya kiutu kwa mamia ya raia wanaohangaika nchini humo.

Maafisa hao wameitaka jumuiya ya kimataifa pamoja na pande za ndani zinazozozana kutowashambulia wafanyakazi wa kimataifa yanayotoa huduma za usamaria mwema kwenye maeneo mbalimbali kwani kwa kufanya hivyo kunakwamisha shughuli wa kuwafikia mamia kwa maelfu ya watu ambao wapo kwenye uhitajio.

Kwa mujibu wa mkuu wa shirika la umoja wa mataifa linalohusika na misaada ya usamaria mwema Bi Valerie Amos kumekuwa na matumizi ya nguvu za kupindukia kama urushaji wa maguruneti na pamoja na makombora yanayotupwa kuanzia angani, ardhini na kwenye maji vitendo ambavyo amedai kuwa vinakwenda kinyume na sheria za kimataifa.

Ametaka kuheshimiwa kwa mipaka ya matumizi ya nguvu na wakati huo huo kujali ustawi wa makundi yanayotaabika ambayo yanapaswa kufikiwa na huduma za usamaria mwema.