Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabalozi wa hisani wa UM kupigia upatu mazingira

Mabalozi wa hisani wa UM kupigia upatu mazingira

Mabalozi wa hisani wa umoja wa mataifa Gisele Bündchen na mwenzio Don Cheadle wanaanza kuchukua hatua za vitendo kushiriki kikamilifu siku ya mazingira  duniani ambayo kilele chake kinafanyika June 5.

Mabalozi hao watashiriki siku hiyo kwa kufanya usafi wakiwa ishara kwamba lazima kufanya mambo kwa vitendo.

Hata hivyo kumeandaliwa mtandao maalumu wa wavuti ambao utatoa fursa kwa wananchi kote duniani kupiga kura  kwa mabalozi wote wawili na wakati huo huo kuweka ahadi zao nini watafanya katika siku hiyo ya mazingira duniani