Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya wahamiaji raia wa Chad wanaowasili jangwani yatia wasiwasi: IOM

Hali ya wahamiaji raia wa Chad wanaowasili jangwani yatia wasiwasi: IOM

Huku maelfu ya watu wakiendelea kukimbia mzozo nchini Libya kila siku kuna wasiwasi kuhusu hali ya wahamiaji kutoka nchini Chad wanaoendelea kuwasili kwenye miji iliyo jangwani ya Faya na Kalait.

Kati ya zaidi ya watu 710,000 waliovuka mpaka wa Libya au waliowasili kwa mashua nchini Italia na Malta karibu wahamiaji 23,000 wamewasili kwa malori kaskazini mwa Chad huku wengi wakiwasili kila siku. Wafanyikazi wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM mjini Faya wanasema kuwa kwa kawaida malori matatu huwasili kila siku yakiwa yamebeba wahamiaji 150 kila lori lakini malori 14 yaliwasili kwa siku moja mapema juma hili huku mengine 14 yakitarajiwa kuwasili wakati wowote