Mikasa ya moto wa msituni inachangia kuongezeka kwa joto duniani:FAO

Mikasa ya moto wa msituni inachangia kuongezeka kwa joto duniani:FAO

Ripoti ya shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa iliyotolewa hii leo kwenye mkutano wa moto kwenye misitu unaofanyika mjini Sun City nchini Afrika Kusini inaonyesha kuwa hata kama mabadiliko ya hali ya hewa huwa yamechangia kuongezeka kwa moto wa msituni kote duniani moto huu wenyewe pia umechangia katika kuongezeka kwa joto duniani.

FAO imetoa wito kwa mataifa kuweka mikakati zaidi katika kukabiliana na moto hasa wa msituni ili kuzuia gesi zinazochangia katika kupanda kwa joto duniani. Mfano ni moto uliotokea mwaka 2009 nchini Australia na kuwaua watu 173 na kuteketeza miji mingi na ule uliotoea urusi mwaka uliopita ambao uliteketeza ekari milioni 2.3. George Njogopa anaripoti

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)