Skip to main content

Ulimwengu unastahili kuwa na tamaa katika kuzisaidia nchi maskini

Ulimwengu unastahili kuwa na tamaa katika kuzisaidia nchi maskini

Rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa amesema kuwa jamii ya kimataifa inastahili kuwa na tamaa katika jitihada zake za kuzikwamua nchi maskini zaidi duniani kutoka kwenye umaskini. Kwa sasa nchi zinazotajwa kuwa masikini zaidi zinakutana mjini Istanbul nchini Uturuki kujaribui kutafuta njia ambazo zinaweza kushirikiana na nchi zingine ulimwenguni ili kujiimarisha kimaendeleo. Nchi hizo 48 duniani huwa zinatajwa kama zinazokabiliwa na umaskini mkubwa, uongozi mbaya pamoja na miundo mbinu mbaya. Joseph Deiss anasema kuwa hatua za dharura zinahitaji kuchukuliwa.

(SAUTI YA JOSEPH DEISS)