Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanafunzi wanahitaji majengo yanayoweza kuhimili majanga

Wanafunzi wanahitaji majengo yanayoweza kuhimili majanga

Utafiti mpya unaonyesha kuwa watoto kwenye nchi zinazokumbwa na majanga ya mara kwa mara wametaja majengo yaliyo salama shuleni kama kitu muhimu wakati kunapotokea majanga. Utafiti huo ulioendeshwa kati ya wanafunzi 600 kwenye nchi 21 unaonyesha kuwa elimu na kupata habari inayohitika ni masuala muhimu katika kupunguza athari zinazosababishwa na majanga pamoja na mabadiliko ya hali hewa kwenye jamii zao. Serikali, wafadhli na mashirika mengine ya kimataifa yataombwa kutia sahihi na kuunga mkono mkataba unaosema kuwa mashule ni lazima yawe salama na elimu haitavurugwa na pia usalama wa mwanafunzi ni lazima upewe kipaumbele wakati na baada ya majanga