Skip to main content

Ban ataka kuwe na usawa katika manufaa ya nishati ya nyuklia na hatari iliyopo

Ban ataka kuwe na usawa katika manufaa ya nishati ya nyuklia na hatari iliyopo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon ametoa wito wa kuwepo kwa mpango katika kusawasisha kwenye manufaa teknolojia ya nguvu za kinyuklia na hatari iliyopo. Akihutubia mkutano kuhusu kuimarisha maandalizi katika ajali ya nishati ya nyuklia Ban amesema kuwa mkasa uliokea kwenye kinu cha Fukushima Daichi nchini Japan umeibua maswali mengi na kuzua hofu kubwa kwa umma. Ban ameonya kuwa ulimwengu huenda ukakumbwa na mikasa kama hiyo hasa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)