Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi masikini zinaweza kuwa na uchumi unaojali mazingira:UNEP

Nchi masikini zinaweza kuwa na uchumi unaojali mazingira:UNEP

Ripoti mpya iliyotolewa na Umoja wa Mataifa imeonyesha kuwa nchi zinazoorodheshwa kuwa maskini zaidi duniani ziko njiani kufikia shabaya kuwa na uchumi unaojali mazingira.

Ripoti hiyo iliyotolewa kwenye mkutano wa 4 wa Umoja wa Mataifa unaojadilia maendeleo ya nchi maskini, imesema kuwa nchi hizo zinaweza kupiga hatua hiyo kwa vile uzalishaji wa hewa chafu angani ni wa kiwango kidogo mno na wakati huo huo zinaendelea kuweka msukomo juu ya sera madhubuti.

Mkutano huo unaofanyika nchini Uturuki unajadilia kwa kina njia na mikakati itayosadia inakwamua nchi hizo maskini. Nchi hizo 48 zinazotambuliwa na Umoja wa Mataifa zinapitia hali mbaya ya umaskini, uongozi mbaya na ukosefu wa miundo mbinu.

Mkutano huo unahudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwemo pia wasomi na wawakilishi wa mashirika ya kiserikali na kiraia.