Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka wanaume kuunga mkono usawa wa kijinsia

Ban ataka wanaume kuunga mkono usawa wa kijinsia

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewataka wanaume kuunga mkono jitihada za kuwainua wanawake akisema kuwa hadi sasa wanawake wanadhulumiwa kwenye jamii nyingi hata baada ya hatua zilizopigwa katika kushirikishwa kwenye masuala ya kijamii , kiuchumi na kisiasa.

Akihutubia mkutano wa wanawake mjini Istanbul nchini Uturuki ambapo alituzwa kwa jitihada zake za kuleta usawa wa kijinsia Ban amesema kuwa bila ya kubadili fikra za wanaume itakuwa vigumu kubadili hali iliyopo sasa.

Ban amesema kuwa wakati wa kipindi chake kama katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa , Umoja wa Mataifa umeangazia masuala ya huduma za kiafya hasa huduma za kiafya kwa wanawake na watoto ikiwa ni lengo la kuokoa maisha milioni 16 ifikapo mwaka 2015.