Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umefungua mkutano wenye lengo la kusaidia nchi masikini

UM umefungua mkutano wenye lengo la kusaidia nchi masikini

Jumuiya ya kimataifa imeungana kutoa wito wa msaada kwa nchi masikini kabisa duniani kwenye mkutano ulioelezewa kuwa mkubwa kabisa wa maendeleo katika muongo huu.

Mkutano huo wa nchi masikini zinazoendelea au LDC’s umeanza rasmi leo mjini Istanbul Uturuki na unaangalia njia za kusaidia kuzikwamua nchi 48 kutoka kwenye umasikini uliokithiri.

Baadhi ya mambo yanayozighubika nchi hizo zinazohitaji msaada ni umasikini wa kupindukia, uongozi mbaua na miundombinu duni. Akifungua mkutano huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema nchi masaikini kabisa zinahitaji msaada kutoka sehemu zingine za dunia.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Na makamu wa Rais wa Tanzania Mohammed Gharib Bilal akizungumza kwenye mkutano huo wan chi masikini amesema

(SAUTI YA MOHAMMED GHARIB BILAL)