Makaburi zaidi ya pamoja yabainika Ivory Coast

9 Mei 2011

Wachunguzi wa haki za binadamu nchini Ivory Coast wamefukua maiti takribani 70 zilizokuwa zimezikwa kwenye makaburi ya pamoja karibu na mji wa Abidjan.

Ofisi ya kamishina mkuu wa haki za binadamu inasema makaburi 10 yalifukuliwa kwenye wilaya ya Yopougon, na mawili kati ya makaburi hayo yalikuwa na maiti 52.

Rupert Colville kutoka ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa anasema uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba mauaji hayo yalifanyika siku moja baada ya kukamatwa na kujisalimisha kwa rais wa zamani wan chi hiyo Laurent Gbagbo.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameonya kwamba baadhi ya uhalifu uliofanyika wakati wa machafuko ya baada ya uchaguzi nchini Ivory Coast unaweza kuhesabiswa kama uhalifu wa kivita.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter