Skip to main content

Historia ya Ulaya Mashariki inatoa funzo kwa demokrasia inayochipuka:Ban

Historia ya Ulaya Mashariki inatoa funzo kwa demokrasia inayochipuka:Ban

Mapinduzi yaliyofanyika nchini tunisia na Misri yanawasilisha moja ya fursa kubwa katika kuelekea demokrasia na haki za binadamu amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Ban Ki-moon ameyasema hayo kwenye mkutano mjini Sofia Bulgaria kuhusu mabadiliko yanayotokea sasa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini. Lakini ameongeza kuwa kuna tofauti kubwa kati ya mapinduzi yaliyotokea Ulaya Mashariki ambayo yalisababisha “kufungwa kwa pazia la chuma” na yanayoendelea hivi sasa.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)-IKO KWENYE ENGLISH CUTS

“Mapinduzi ya mwaka 1989 yalikuwa mepesi, hayakuwa na umwagaji damu. Tunachokiona Libya, Bahrain, yemen, syria na kwingineko yoye yameghubikwa na umwagaji damu.”