Usafirishaji haramu wa watu umezidi Thailand:IOM

6 Mei 2011

Kumekuwa na ongezeko kubwa la usafirishaji haramu binadamu nchini Thailand nchi ambayo inasifika kwa umashuhuri wake wa uzalishaji kwa wingi wa samaki.

Thailandni mzalishaji mkubwa wa samaki na inatajwa kuwa na kiwanda kikikubwa chenye mtaji wa mabilini ya dola.

Katika ripoti yake iliyochapishwa juma hili, shirika la kimataifa la uhamiaji limesema kuwa vitendo vya usafirishaji haramu binadamu vinaendelea kumea mizizi na katika siku za hivi karibuni kiwango hicho kimepindukia mipaka.

Ripoti hiyo ambayo tayari imewasilishwa pia kwa mammlaka za Thailand inataka kuchukuliwa kwa hatua za haraka kudhibiti hali na imetoa mapendezo kadhaa ambayo yanapaswa kuzingatiwa.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter