Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO na Nigeria wazindua mpango mpya wa elimu

UNESCO na Nigeria wazindua mpango mpya wa elimu

Shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO limeafikia makubalino na serikali ya Nigeria kwenye mpango utakaogharimu dola milioni sita ambapo watu wazima na vijana watapata elimu kote nchini.

Makubalino hayo yalitiwa sahihi hii leo mjini Paris na mkurugenzi mkuu wa UNESCO Irina Bokova na waziri wa elimu nchini Nigeria Ruqayyatu Ahmed Rufa’i.

Inakadiriwa kuwa watu wazima milioni 50 hawajui kusoma wala kuandika nchini Nigeria huku watoto milioni 8.6 walio na umri wa kujiunga na shule za msingi wakiwa bado hawaendi shuleni. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)