Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Marekani yahofia kupanda kwa bei ya chakula:FAO

Marekani yahofia kupanda kwa bei ya chakula:FAO

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Clinton amesema kuwa ulimwengu unahitaji kushirikiana ili masoko yapate kufanikiwa kama njia ya kukabiliana na tatizo la kupanda kwa bei ya vyakula.

Clinton aliyasema hayo kwenye makao makuu ya shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa ambapo alihutubia mashirika ya chakula ya Umoja wa Mataifa yaliyo mjini Rome na wawakilishi kupitia kwa mwaliko wa mkurugenzi mkuu wa shirika la FAO Jacques Diouf

(SAUTI YA HILARY CLINTON)