Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu waendelea kukimbia machafuko Libya:IOM

Maelfu waendelea kukimbia machafuko Libya:IOM

Shirika la kimataifa la uhamaijai IOM linasema kuwa maelfu ya watu wanazidi kukimbia mzozo nchini Libya kila siku huku wasiwasi ukiibuka kuhusu hali ya raia wa Chad wanaowasili kwenye miji ya jangwani ya Faya na Kalait.

IOM inasema kuwa kwa kawaida malori matatu yaliyo na watu 150 kila lori yanawasili kwenye mji wa Faya kila siku lakini mapema juma hili malori 14 yaliwasili kwa siku moja.

Pia malori mengine 14 yanayokisiwa kuwasafiri akina mama na watoto yanaripotiwa kuwa safarini kwenda mji wa Faya na huenda yakawasili wakati wowote. Jumbe Omari Jumbe na mengi zaidi.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)