Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukiukwaji wa haki za binadamu Ivory Coast kuchunguzwa

Ukiukwaji wa haki za binadamu Ivory Coast kuchunguzwa

Tume ya kimataifa ya kuchunguza hali nchini Ivory Coast imewasili nchini humo na kwa sasa makamishina wa tume hiyo wako mjini Abidjan ambapo wanakutana na washikadau huku wakitarajiwa kuyazuru maeneo mengine ya nchi juma lijalo.

Tume hiyo ina wanachama 12 wakiwemo washauri wa jinsia , wataalu wa masuala ya watoto na mizozo pamoja na wataaalumu wa kijeshi na wa kiusalama. Rupert Colville kutoka afisi ya haki za binadamu anaeleza jukumu la tume hiyo.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

Amesema pia kuwa wafanyikamzi kutoka ofisi ya haki za binadamu walio nchini Ivory Coast wanachunguza madai ya ukiukaji wa haki za binadamu kwenye wilaya ya Yopougon ambapo inakadiriwa watu 40 waliuawa mapema juma hili.