Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wachunguzi wa haki za binadamu wa UM wataka ukweli kuhusu kifo cha Osama

Wachunguzi wa haki za binadamu wa UM wataka ukweli kuhusu kifo cha Osama

Wachunguzi wa masuala ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wanataka ukweli kutolea kuhusu kuuawa kwa Osama Bin Laden.

Christof Heyns mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji yaliyo kinyume cha sheria na Martin Scheinin mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na kulinda haki za binadamu wakati wa kupambana na ugaidi wanasema kuwa wanataka kujua ikiwa matumizi ya nguvu dhidi ya Osama Bin Laden yalizingatia viwango vya kimataifa vya sheria za haki za binadamu.

Wanasema kuwa ni muhimu kufahamu ikiwa mipango ya kumsaka Osama ilitoa nafasi ya kumkamata. Prof Heyns anasema kuwa hata kama matumizi ya nguvu yanaweza kuruhusiwa ili kulinda maisha magaidi wanastahili kuchukuliwa kama wahalifu kwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani.

(SAUTI YA PROF HEYNS)

Osama Bin Laden ambaye alipanga mashambulizi ya septemba 11 mwaka 2001 nchini Marekani aliuawa mapema juma hili na vikosi vya Marekani.