Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhamiaji ni mada itakayojadiliwa Istanbul kwenye mkutano wa LDC

Uhamiaji ni mada itakayojadiliwa Istanbul kwenye mkutano wa LDC

Mkuu wa shirika la umoja wa mataifa linalohusika na uhamiaji William Lacy Swing ataweka kipaumbele cha pekee kwa kujadilia suala la mahusiano yaliyopo baina ya uhamiaji na maendeleo wakati wa mkutano wa kilele wan chi zinazoendelea unaotazamiwa kuanza wiki ijayo huko Instanbul Uturuki.

Katika taarifa yake juu ya mkutano huo Mkurugenzi huyo mkuu ameeleza kuwa kwa mara ya kwanza mkutano huo unatambua nafasi ya wahamiaji wa ngambo wanavyoweza kukuza pato la taifa kwa nchi zao za asili,na hivyo kuingizwa kwa suala hilo kwenye mkutano huo ni hatua inayopaswa kupigiwa mkono.

Mkutano huo kwa mara ya kwanza umepanga kujadilia kwa kina mtitiriko wa mapato yanayorejeshwa nyumbani toka kwa wale wanaofanya kazi nje ya nchi zao.

Benki ya dunia katika taarifa yake ya hivi karibuni imesema nchi zinazoendelea katika kipindi cha mwaka 2009 zilipokea kiasi cha  dola za kimarekani  bilioni 24 kiwango ambacho kiliizidi makadirio yaliyowekwa hapo kabla.