Wanawake ni muhimu kushiriki masuala ya demokrasia

5 Mei 2011

Maafisa wa ngazi za juu kwenye Umoja wa Mataifa wamesisitiza umuhimu wa kuwashirikisha wanawake katika kutoa maamuzi wakisema kuwa demokrasia na usawa wa kijinsia vyote ni kitu kimoja.

Akiongea kwenye mkutano kuhusu usawa wa kijinsia na demokrasia uliondaliwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki –moon amaesema kuwa kushirikishwa kwa wanawake kunaimarisha demokrasia akiongeza kuwa demokrasia ndicho chanzo cha usawa wa kijinsia.

Ban ameongeza kuwa kushirikishwa kwa wanawake kunatoa nafasi ya kujadiliwa kwa haki za binadamu na kuwainua wanawake, kuwafanya wanawake kuungana na kuwarahisishia wanawake kuelewa haki zao za kisiasa , uchumi na haki za kijamii.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter