Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wakaribisha kuanza kesi ya FDLR Ujerumani

UM wakaribisha kuanza kesi ya FDLR Ujerumani

Afisa wa Umoja wa mataifa aliye msitari wa mbele katika juhudi za kukabiliana na makosa ya ubakaji yaliyofanyika wakati wa vita lamekaribisha kuanza kwa kesi ya Wanyarwanda wawili nchini Ujerumani wanaoshutumiwa kuagiza mauaji ya halaiki na ubakaji wa watu wengi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Ignace Murwanashyaka na Straton Musoni ambao kesi yao imeanza jana wanakabiliwa na makosa 39 kila mmoja ya uhalifu wa vita na 26 ya uhalifu dhidi ya ubinadamu yaliyotekelezwa Mashariki mwa Congo mwaka 2008 hadi 2009.

Afisa huyo Margot Wallstrom ambaye ni mwakilishi wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili wa kimapenzi katika maeneo ya vita, ameipongeza serikali ya Ujerumani kwa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani wahalifu hao. Amesema kesi hiyo ni ishara ya wazi kwamba hakuna pepo kwa washukiwa wa uhalifu na hakuna msamaha wala kukwepa mkono wa sheria kwa ubakaji vitani.