Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA imeandaa mashindano ya kwanza ya marathon Gaza

UNRWA imeandaa mashindano ya kwanza ya marathon Gaza

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa msaada kwa Wapalestina UNRWA leo umefanya kwa mara ya kwanza kabisa mashindano yam bio za marathon kwa ajili ya kuchangisha fedha zitakazotumika kuendesha michezo mikubwa ya kiangazi iitwayo Gaza summer games.

Mbio hizo zimeshirikisha eneo lote la Ukanda wa Gaza, kuanzia Beit Hanoun hadi Rafah, ambapo watoto wamekimbia kwa kupokezana, huku watu wazima waliojumuisha wanariadha mashuhuri wa Gaza wanaojinoa kwa ajili ya mashindano ya olimpiki hadi wafanyakazi wa kimataifa.

Mashindano hayo ni ya marathoni kamili, nusu marathon au kilometa 10. Chis Gunnes wa UNRWA anasema mashindano yamekuwa ya mafanikio na kutoa picha halisi ya watu wa Gaza.

(SAUTI YA CHRIS GUNNES)