Uchuguzi wa haki za binadamu waendeshwa Somalia

4 Mei 2011

Shirika la kuchunguza utekelezwaji wa haki za binadamu la Umoja wa Mataifa UPR limeendesha uchunguzi wake nchini Somalia katika kubaini yanayojiri nchini humo kuhusiana na kuheshimu haki za binadamu.

Kumekuwa na madai ya ukiukji mkubwa wa haki za binadamu ambao umeshuhudiwa Kusini na kati kati mwa Somalia kama vile haki ya kujieleza, matumizi ya mahaka katika kukandamiza , vitisho dhidi ya watetesi wa haki za binadamu na ukiukaji mwingine wa haki za binadamu.

Wakati huohuo katibu mkuu wa NUSOJ Faruk Osman ametoa ushauri kwa ujumbe wa serikali ya ya mpito ya Somalia ambao kwa sasa uko mjini Geneva kukakikisha utekelezwaji wa mikataba ya kimataifa inayohusiana na haki za binadamu ambayo Somalia ni mwanachama.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter