Tamasha la amani lafanyika Gaza

Tamasha la amani lafanyika Gaza

Kumekuwa na hali ya shamra shamra na nderemo huko Gaza wakati mjumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa Daniel Barenboim alipoendesha tamasha maalumu lililolenga

kuhamasisha amani na upendo katika maeneo yaliyoharibiwa na machafuko ya vita. Bwana Barenboim hivi karibuni iliunda bendi maalumu kwa ajili ya Gaza, bendi ambayo imewajumuisha wasanii mbalimbali wa Ulaya kwa shabaya ya kuendesha matamasha ya kuhamasisha amani na upendo.

Akizungumzia tamasha hilo mwana amani huyo ameeleza kuwa lilenga kuwaletea ujumbe wa amani kwa wananchi wa Gaza.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, amepongeza hatua hiyo akisema kuwa ni faraja kubwa kuona wale wenye vipaji wakitumia fursa hiyo kuwajali wale wenye matatizo.