UM kuondosha dawa ambazo ni hatari kwa mazingira

4 Mei 2011

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira UNEP limeitangaza dawa inayotumika kunyunyuziwa kwenye mimee kwa ajili ya kuu vijidudu kuwa ni dawa hatari na lazima iondolewe kwenye mzunguko wa soka.

Dawa hiyo inayofahamika kitaalamu kama endosulfan huenda ikaondolewa katika kipindi cha mwaka mmoja ujao kuanzia sasa, na tayari wataalamu waliokutana huko Geneva wameafikia hatua hiyo.

Jumla ya wawakilishi wan chi 127 waliokutana huko Geneva, kuanzia April 25 hadi 29 wameunga mkono kuwa lazima dawa hiyo iondolewe haraka kwani matumizi yake yanaleta taswira mbaya kwenye uso wa dunia.

Mathara yanayotajwa kusababishwa na matumizi ya madawa hayo ni pamoja na kuharibu mazingira na kuleta uharibifu mkubwa kwa maisha ya binadamu na viumbe vingine.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter