Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idara ya kulinda amani ya UM yajadili sheria

Idara ya kulinda amani ya UM yajadili sheria

Wakuu wa masuala ya utawala wa sheria wa vitengo mbalimbali vya Umoja wa mataifa wanakutana mjini New Yory kwenye makao makuu ya Umoja wa mataifa kwa juma zima kujadili changamoto na msaada wa kisheria katika shughuli za kulinda amani.

Mkutano huo ulioandaliwa na idara ya operesheni za kulinda amani ya Umoja wa Mataifa unawaleta pamoja maafisa wanaohusika na masuala ya magereza, washauri wa kisheria, wakuu wa polisi wa Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa sheria wakichanganua mada ya utawala wa sheria katika shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa.

Jairus Gilbert Omondi ni afisa wa kurekebisha tabia katika magereza kwenye mpango wa Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika wa kulinda amani Darfur UNAMID, anafafanua ajenda ya mkutano wao.

(SAUTI YA JAIRUS GILBERT OMONDI)