Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wagonjwa wa kisukari wana hatari ya kupata TB

Wagonjwa wa kisukari wana hatari ya kupata TB

Watu wenye matatizo ya kisukari wanakabiliwa na hatari ya kupata ugonjwa wa kifua kikuu (TB) kuliko ambao hawana kisukari. Hii ni kwa mujibu wa matokeo ya utafiti yaliyochapishwa leo na shirika la afya duniani WHO.

Utafiti huo uliofanywa katika jamii zilizo na matatizo ya huduma za afya kwenye mpaka baina ya Mexico na Marekani umebaini kwamba watu wenye kisukari wanakabiliwa na hatari mara tatu hadi tano ya kuambukizwa kifua kikuu ukilinganisha na watu ambao wanaishi katika eneo hilohilo lakini hawana kisukari. George Njogopa anaripoti

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)