Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM inaendelea kuwahamisha wahamiaji Misrata

IOM inaendelea kuwahamisha wahamiaji Misrata

Takriban watu 800 wakiwemo wahamiaji waliokwama na majeruhi 50 ambao ni raia wamehamishwa leo na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kutoka mjini Misrata Libya licha ya mapigano makali na makombora yanayovurumishwa.

Wafanyakazi wa IOM wakiwa na boti ya Red Star One wanasema iliwabidi kusubiri kwa saa tatu baada ya kutia nanga mjini hapo wakisubiri watu na kusalia na muda mfupi tuu kuwaokoa.

Maroketi yanayorushwa na mapigano yanayoendelea yamezuia boti za IOm kutia nanga kwa siku tano. Watu 1000 ambao ni wahamiaji wamelazimika kuhamishwa na IOm kukimbia machafuko hayo kama anavyofafanua Jumbe Omari Jumbe wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)