Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwendesha mashitaka wa ICC kuomba kibali cha kukamatwa watu watatu Libya

Mwendesha mashitaka wa ICC kuomba kibali cha kukamatwa watu watatu Libya

Mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC Luis Moreno-Ocampo leo ameliarifu baraza la usalama la Umoja wa mataifa kwamba katika wiki chache ataomba majaji wa ICC kutoa kibali cha kukamatwa watu watatu kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu uliotekelezwa Libya tangu Februari 15 mwaka huu.

Amesema kwa mujibu wa ushahidi ndio wahusika wakuu wa uhalifu uliofanyika. Hata hivyo amesema majaji wataamua ama kukubali, kukataa au kutaka ushahidi zaidi. 

Hali nchini Libya ilipelekwa kwa mwendesha mashitaka wa ICC baada ya baraza la usalama kupiga kura na kupitisha chini ya azimio namba 1970 hapo Februari 20 mwaka huu. 

Ocampo amesema kwa mujibu wa ushahidi uliokusanywa hadi sasa uhalifu dhidi ya ubinadamu umefanyika na uanaendelea nchini Libya, kwa kushambulia raia wasio na silaha ikiwa ni pamoja na mauaji, utesaji na unyanyasaji katika miji mingi ya nchi hiyo. 

(SAUTI YA MORENO OCAMPO)