Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya watu duniani kufikia bilioni 16 mwaka 2100

Idadi ya watu duniani kufikia bilioni 16 mwaka 2100

Ongezeko la idadi ya watu linaweza kufikia bilioni 16 ifikapo mwaka 2100 imesema ripoti mpya ya kitengo cha Umoja wa Mataifa cha idadi ya watu.

Ifikapo karne ya 22 idadi ya watu duniani itakuwa ndogo kiasi cha bilioni 6, idadi ambayo tumekwishaipita au idadi kubwa ya bilioni 16 ambayo itasababisha upungufu na matatizo ya chakula.

Hania Zlotnick , mkuu kitengo cha idadi ya watu cha Umoja wa Mataifa anasema kinachotarajiwa ni kwamba idadi ya watu itaendelea kuongezeka katika karne hii na kufikia takribani bilioni 10 kutoka idadi ya sasa ambayo ni karibu watu bilioni saba duniani.

Kitakachotathimini idadi ya watu watakaokuwa hai ifikapo mwaka 2100 ni kiasi cha watoto watakaokuwepo kwenye familia ya kawaida katika miaka 90 ijayo. Matarajio ya idadi ya watu yanapatikana kwenye marejeo ya tathimini ya mwaka 2010 yaliyotayarishwa na kitengo cha Umoja wa Mataifa cha idadi ya watu.

Ripoti inasema nchi 39 zinazo na kiwango kikubwa cha kuzaa ziko Afrika , lakini karibu 20 ziko Amerika Kusini, Asia na Ocenia.