Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu kadhaa wanashikiliwa na serikali na upinzani Libya

Watu kadhaa wanashikiliwa na serikali na upinzani Libya

Watu zaidi ya 180 wanashikiliwa na majeshi ya serikali nay a upinzani nchini Libya imesema tume ya Umoja wa mataifa ya inayochunguza ukiukaji wa haki za binadamu nchini Libya.

Mjini Tripoli serikali ya Libya inawashikilia watu 86 wakiwemo waandishi habari 18. Nako Benghazi majeshi ya upinzani yanawashikilia watu 76 miongoni mwao wanajeshi wa serikali na wanaodaiwa kuwa askari mamluki.

Tume hiyo imetoa wito wa kuwaachilia mahabusu hao kwa misingi ya haki za binadamu, na imeukumbusha uongozi wa Libya haja ya kuzingatia sheria na viwango vya kimataifa wanapowatendea na kuwashikilia mahabusu hao.

Tume hiyo ilizuru hospitali na mahabusu kwenye miji kadhaa ya nchi hiyo ikiwemo Tripoli na Benghazi. Pia imekuwa na mazungumzo na maafisa wa serikali pamoja na wawakilishi wa baraza la upinzani la kitaifa. Ripoti ya tume hiyo itawasilishwa kwa baraza la haki za binadamu kwenye kikao chake kijacho Juni mwaka huu.