Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Biashara lazima zizingatie maslahi na kulinha haki za watoto:UNICEF

Biashara lazima zizingatie maslahi na kulinha haki za watoto:UNICEF

Mashirika yakiwemo shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF na lile la Save the Children yanasema kuwa biashara inastahili kuchangia katika kuweka viwango vya kibiashara vya kimataifa kuambatana na haki za watoto.

Kwenye uzinduzi huo unaofanyika hii leo kupitia mtandao ni bayana kuwa sekta za kibinafsi zinaweza kuboresha haki za watoto kwa kuweka viwango vya biashara zinazozingatia maslahi ya watoto. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Mpango huo ambao umepangwa kuzinduliwa mwezi Novemba unatajwa kuwa ni hatua muhimu na ya kwanza kushuhudiwa ikiweka misingi na miiko ambayo itayalazimu makampuni ya kibiashara kuweka mazingira yatakayohakikisha yanaheshimu haki za binadamu.

Zingatio kubwa kwenye mkakati huo ni kuona kwamba kuanzia maeneo ya kazi, viwandani, na maeneo mengine ya kiutendaji yanazingatia na kuheshimu haki za watoto.

Inaaminika kuwa kupitia mchango wa makampuni binafsi, kunaweza kupigwa hatua kubwa kwenye ufikiaji malengo ya kuheshimu kwa haki za watoto, hasa kutokana na ushawishi wake wa kibiashara na namna inavyoendesha mambo.