Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali Ivory Coast bado inatia wasiwasi kwa maelfu:UNHCR

Hali Ivory Coast bado inatia wasiwasi kwa maelfu:UNHCR

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa hali nchini Ivory Coast kwa maelfu ya raia wa nchi hiyo inatia wasiwasi hata baada ya kuimarishwa kwa usalama kote nchini.

UNHCR inasema kuwa idadi ya wakimbizi wa ndani imepungua kutoka wakimbizi 35,000 mwishoni mwa mwezi Machi hadi wakimbizi 14,000 juma lililopita. Hata hivyo kuna uhaba mkubwa wa chaKula.

Wakimbizi wa ndani waliokuwa wameweka kambi kwenye makao ya kimishenari ya Cathloc wameamua kurejea makwao anavyoeleza Adrian Edward kutoka UNHCR.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)