Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pande hasimu Libya zimetakiwa kuruhusu meli ya misaada

Pande hasimu Libya zimetakiwa kuruhusu meli ya misaada

Mashirika ya kimataifa ya kutoa huduma za kibinadamu likiwemo shirika la kimataifa la uhamiaji IOM na kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu ICRC wanaendelea kutoa usaidizi mji Benghazi nchini Libya.

ICRC imesaidia katika kuwahamisha wahamiaji 2300 huku ikiwa na mipango ya kupeleka misaada kwenye mji wa Misrata. Hata hivyo ICRC inakumbwa na wasiwasi wa mabomu yaliyo ardhini ambayo bado hayajalipuka.

Inasema kuwa itazindua kampeni za kuhamasisha umma kuhusu mabomu ambayo bado hayajalipuka. Kulingana na Jumbe Omari Jumbe IOM inatoa wito kwa pande zilizo kwenye mzozo nchini Libya kuruhusu mashua yake kutia nanga mjini Misrata ili kuwaokoa karibu wahamiaji 1000 waliokwama mjini humo na raia wengine walio na majeraha mabaya.

Mashua hiyo imekuwa ikisubiri tangu tarehe 30 mwezi Aprili kutia nanga mjini Misrata.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)