Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yazitaka nchi za Asia ya Kati kushirikiana kwa karibu zaidi

FAO yazitaka nchi za Asia ya Kati kushirikiana kwa karibu zaidi

Katika hali ambayo sokomoko la mabadiliko ya tabia nchi likiendelea kuziandama nchi mbalimbali, huku pia kukishuhudiwa kupanda kwa bei ya vyakula.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la chakula la kilimo FAO Jacques Diouf amezitaka nchi zilizoko kwenye eneo la Asia ya Kati kuweka makubaliano ya pamoja ili kurahisha usafirishaji wa bidhaa za kilimo miongoni mwao.

Akizungumza kwenye kongamano la kiuchumi katika mji wa Astana, Kazakhstan, Diouf  amezungumzia hali inavyoliandamana eneo hilo ambalo linakabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa chakula cha kutosha hivyo ametaka kuweka nguvu ya pamoja kwa shabaya ya kujiongezea usalama wa chakula hicho.

Nchi nyingi kwenye ukanda huo, zinategemea zaidi vyakula aina ya nafaka vinavyoingizwa toka nchi za ng'ambo lakini Kazakhstan ni nchi pekee yenye unafuu wa kuzalisha chakula kingi zaidi.

Amesema kwa kupitia makubaliano ya pamoja na uanzishwaji mashirikiano ya kikanda, kunaweza kutoa mchango mkubwa ambao utahakikisha kuwepo kwa usalama wa chakula.