Skip to main content

Tumbaku inaweza kuua watu milioni 1:UM

Tumbaku inaweza kuua watu milioni 1:UM

Kuna uwezekano wa watu zaidi ya bilioni moja wakapoteza maisha ndani ya karne hii kutokana na matumizi ya tumbaku, iwapo juhudi za haraka hazitachukuliwa kunusuru hali hiyo hasa mataifa yenye kipato cha chini na wastani.

Kulingana na Douglas Bettcher ambaye ni mkurugenzi wa shirika la afya duniani WHO kwenye kitengo cha tumbaku, nchi zenye kipato cha wastani ya chini zinapaswa kuhakikisha kwamba zinachukua mkondo mpya wa uwekaji wa sheria na kanuni kwa ajili ya kukabiliana na hali ya matumizi ya tumbaku.

 

Ametaja pia tayari baadhi ya mataifa hayo yameanza kukumbana na athari hizo. Mtaalamu huyo amesema kuwa kwa kila mwaka watu wanaofikia milioni 6 hupoteza maisha kutokana ama kwa uvutaji wa tumbaku wa moja kwa moja ama maambukizi yaletwayo na uvutaji wa hadharani.