Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Wapalestina unahitaji kuleta amani:Ban

Umoja wa Wapalestina unahitaji kuleta amani:Ban

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa shughuli za kuleta mapatano miongoni mwa wapalestina lazima zifanyike kwa njia ambayo itachangia kuwepo kwa amani na usalama.

Hii ni baada ya makundi ya Fatah na Hamas kutangaza kuwa yameafikiana makubalino ya kuunda serikali ya umoja na kundaa uchaguzi mwaka huu.

Akiongea kwa njia ya simu na naibu waziri mkuu nchini Israel ambaye pia ni waziri wa ulinzi Ehud Barak, Ban amezungumzia maafikiano ya hivi majuzi kati ya makundi hayo mawili chini ya uongozi wa Misri na mpango wa amani wa mashariki ya kati.

Ban amesema kuwa Umoja wa Mataifa utachunguza maafikiano hayo kwa kina. Ban ni miongoni mwa maafisa wa Umoja wa Mataifa ambao wamekuwa wakitoa wito kwa makundi hayo kuachana na tofauti zao na kwa pamoja kutatua matatizo yanayowakumba Wapalestina.