Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufadhili wa mabadiliko ya hali ya hewa uchangie uwekezaji:UM

Ufadhili wa mabadiliko ya hali ya hewa uchangie uwekezaji:UM

Afisa wa ngazi ya juu katika masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa kwenye Umoja wa Mataifa amesema kuwa ufadhili mpya utakaozisadia nchi zinazoendelea kukabiliina na mabadiliko ya hali ya hewa unahitaji kuwatia moyo wawekezaji wa kibinafsi.

Katibu mkuu wa shirika linalohusika na mabadiliko ya hali ya hewa la Umoja wa Mataifa (UNFCCC) Christiana Figueres amesema kuwa uwekezaji katika sekta za kibinafsi ni muhimu katika kuhakikisha kupungua kwa hewa zinazochafua mazingira kwa nchi maskini.

Kuzinduliwa kwa ufadhili huo ni kati ya makubaliano yaliyoafikiwa kwenye mkutano wa Cancun unaoonyesha kuwa mataifa yanaweza kuchukua hatua zifaazo hata kwenye mkutano wa mwaka huu mjini Durban. Kwenye mkutano wa Cancun mataifa tajiri yalikubaliana kuchangisha dola bilioni 100 kila mwaka hadi mwaka 2020 kufadhili mpango huo.