Skip to main content

Maeneo ya mizozo kujadiliwa kwenye baraza la usalama:Gerard

Maeneo ya mizozo kujadiliwa kwenye baraza la usalama:Gerard

Ufaransa ambayo itakuwa ni rais wa mzunguko kwenye baraza la usalama mwezi huu wa Mai inasema itajikita katika maeneo yanayoghubikwa na machafuko mwezi huu.

Itamulika kazi ya mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu kuhusu suala la Libya, pia itaangalia jukumu la Umoja wa Mataifa nchini Sudan baada ya Sudan Kusini kuwa taifa huru na mkutano kuhusu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na ni ajenda zitakazokuwa msitari wa mbele kwenye mjadala wa baraza la usalama.

Balozi wa Ufaransa kwenye Umoja wa Mataifa ni Gerard Araud akizungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa anafafanua kuhusu ajenda hizo za mwezi Mai na kusema mabadiliko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni muhimu yakafanyika sasa kwani Umoja wa Mataifa hauwezi kusalia huko daima.

(SAUTI YA GERAD ARAUD)