Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID imetangaza mipango ya kibinadamu kusaidia Darfur

UNAMID imetangaza mipango ya kibinadamu kusaidia Darfur

Mwakilishi maalumu wa vikosi vya pamoja vya Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika kulinda amani Darfur UNAMID Ibrahim Gambari amezindua mradi maalumu wenye lengo la kuongeza fursa kwa mashirika ya msaada wa kibinadamu ili kuwafikia maelfu ya watu katika jamii zilizoathirika na vita na ambazo ni vigumu kufikika kwenye jimbo la Darfur.

Mradi huo ambao umeandaliwa na UNAMID kwa ushirikiano na shirika la kuratibu masuala ya kibindamu la OCHA utafanyika kwa wiki tatu ambapo vijiji vilivyokuwa havifikiki sasa   vitatembelewa.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini El Fasher Gambari amesema hivi sasa kipaumbele chake ni kuhakikisha inasaidia mashirika ya misaada na NGO's kuweza kufika katika maeneo yasiyofikika na kutoa msaada unaohitajika.