Skip to main content

Uwekezaji usaidie ajira na hali ya maisha:UNCTAD

Uwekezaji usaidie ajira na hali ya maisha:UNCTAD

Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na maendeleo UNCTAD kuhusu uwekezaji wa moja kwa moja wa nje (FDI) katika nchi 48 masikini kabisa duniani, imetaka kuwe na mabadiliko ya mtazamo ili kusaidia kutoa nafasi za ajira pamoja na kuinua hali ya maisha katika nchi hizo, kuziwezesha kuzalisha bidhaa nyingi na zilizo tofauti.

Ripoti hiyo inayoitwa uwekezaji wa moja kwa moja wa nje katika nchi masikini , funzo lililopatikana katika muongo kuanzia 2001-2010 na njia ya kuweza kusonga mbele, ina lengo la kuchangia katika mjadala utakaofanyika wiki ijayo kwenye mkutano wa nne wa Umoja wa Mataifa kuhusu mataifa ambayo hayajaendelea utakaofanyika mjini Istanbul Uturuki .

James Zhan ni mkurugenzi wa kitengo cha uwekezaji cha UNCTAD.

(SAUTI YA JAMES ZHAN)

Pia amesema ripoti hiyo imependekeza kuanzishwa kwa mfuko wa maendeleo ya miundombinu kwa nchi masikini ambao utasaidia kuboresha hali katika mataifa hayo ili kuchagiza na kuvutia zaidi wawekezaji. Miundombinu hiyo ni pamoja na nishati ya umeme, barabara, reli, na mtandao wa internet.