Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matumizi ya nguvu yanachochea ghasia Uganda:Pillay

Matumizi ya nguvu yanachochea ghasia Uganda:Pillay

Watu takribani wanane wameuawa nchini Uganda na wengine wengi kujeruhiwa wakati majeshi ya usalama yalipowakabili waandamanaji waliokuwa wakipinga kupanda kwa gharama za maisha.

Kwa mujibu wa taarifa zilizokusanywa na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa takribani watu 250 wakiwemo wanawake na watoto wamejeruhiwa na wengine zaidi ya 580 wamekamatwa wakati wa machafuko hayo yaliyoanza  wiki tatu zilizopita.

Kamishna mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay ameitaka serikali ya Uganda kusitisha matumizi ya nguvu kupita kiasia dhidi ya waandamanaji na kuwakandamiza wanasiasa wa upinzani akiwemo dr Kizza Besigye. Kiongozi huyo wa upinzani amearifiwa kukamatwa mara tatu, kupigwa risasi mkononi na wiki iliyopita alipuliziwa pilipili machoni.

Pillay amesema jeshi la pili na la ulinzi la Uganda kuingilia maandamano hayo kumesababisha kukikukwa haki za binadamu ikiwemo ya kuishi, uhuru wa kukusanyika na wa kujieleza. Pillay ameitaka serikali kufanya uchunguzi wa kina na huru dhidi ya ukiukaji wa haki za binadamu uliotekelezwa na majeshi ya ulinzi na usalama.