Kwa waliopoteza maisha haki imetendeka A. Mashariki pia

2 Mei 2011

Kifo cha kiongozi wa Al Qaeida Osama Bin Laden pia kimetoa afueni kwa maelfu ya watu kwenye nchi za Afrika ya Mashariki hususani Kenya na Tanzania ambako mamia ya watu waliuawa katika shambulio la kwanza la kigaidi eneo hilo mwaka 1998.

Nchini Kenya tarehe 7 Agosti 1008  saa nne na nusu asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki ubalozi wa Marekani ulilipuliwa na shambulio na kigaini baada ya lori lililokuwa na mabomu kulipuka ubalozini hapo, watu 212 waliuawa na wengine 4000 kujeruhiwa, taarifa za kifo chake zimepokelewa vipi? Jason Nyakundi anaarifu

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Nako Dar es salaam Tanzania saa nne na dakika arobaini asubuhi saa za Afrika Mashariki siku hiyohiyo kwenye ubalozi wa Marekani lori lililokuwa na mabomu lililipuka, watu 11 walipoteza maisha na wengine 85 kujeruhiwa, leo kutangazwa kwa kifo chake kumezua hisia tofauti.

(MAONI OSAMA TZ)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter