Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aitaka dunia kuwakumbuka wahanga wa ugaidi katika wakati huu ambao Osama Bin Laden amekufa

Ban aitaka dunia kuwakumbuka wahanga wa ugaidi katika wakati huu ambao Osama Bin Laden amekufa

Mwanzilishi na kiongozi wa mtandao wa kigaidi wa kimataifa wa Al Qaeda , bwana Osama Bin Laden ameuawa na majeshi ya Marekani nchini Pakistan.

Akitangaza kifo hicho Rais wa Marekani Barak Obama amesema Osama aliuawa baada ya majibiza no ya risasi kwenye eneo la Abbottabad Kaskazini mwa Islamabad na Marekani kuchukua mwili wake ambao sasa unasemekana kuzikwa baharini. Obama amesema kwa maelfu ya watu waliopoteza maisha kwa mashambulio ya kigaidi ya Osama haki imetendeka.

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akizungumzia kuhusiana na tukio hilo amesema amelikaribisha na kwamba Umoja wa Mataifa unapinga aina yoyote ile ya ugaidi katika dunia hii.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Bin Laden anashutumiwa kwa mashambulizi kadhaa ya kigaidi duniani ikiwemo kubwa kabisa katika ardhi ya Marekani mjini New York na Washington Septemba 11 2001. Kifo chake kimeelezwa kuwa pigo kubwa kwa kundi la Al Qaeda lakini kuna hofu kwamba huenda kukatokea mashambulizi ya kulipiza kisasi.