Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani vikali shambulio la bomu Morocco

UM walaani vikali shambulio la bomu Morocco

Baraza la usalama na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa pamoja wamelaani vikali mashambulio ya mabomu kwenye mhagawa mjini Marrakech nchini Morocco ambako watu takribani 20 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa.

Duru za habari zinasema mchanganyiko wa raia wa Morocco na wa kigeni ni miongoni mwa waliokufa kwenye shambulio hilo ambalo lilitokea jana asubuhi . Katika taarifa iliyotolewa leo wajumbe wa baraza la usalama wametuma salamu za rambirambi kwa familia ya waliokufa, serikali na watu wa Morocco.

Wamesema ugaidi katika mfumo wowote ule ni moja ya tishio kubwa katika amani na usalama wa kimataifa, na vitendo vyovyote vya kigaidi ni kosa la jinai na havikubaliki, bila kujali nani amefanya, kwa nini, wali na lini. Kwa upande wake Katibu Mkuu Ban amerejea kupinga matumizi ya ghasia na mashambulizi dhidi ya raia wasio na hatia.