Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM kusaidia upatikanaji wa ajira kwa wananchi Haiti

IOM kusaidia upatikanaji wa ajira kwa wananchi Haiti

Shirika la umoja wa mataifa linalohusika na uhamiaji IOM, linatazamiwa kuendelea utoaji huduma inayohusiana na masuala ya UKIMWI nchini Haiti katika kipindi chote cha mwaka huu 2011.

Hatua hiyo inafuatia kupatikana kwa fungu la fedha kiasi cha dola za kimarekani 20,000 zilizotolewa na mpango wa dharura wa rais wa marekani PEPFAR. Kiasi hicho cha fedha kinatazamiwa kuwafaidia mamia ya wananchi wa Haiti walio hatarini kuangukia kwenye maambukizi ya ukimwi ambao kusaidiwa kutafutiwa ajira.

 

IOM imeeleza kuwa uanzishwaji wa ajira za muda kunatoa nafasi kubwa ya unafuu wa maisha kwa familia nyingi ambazo bado zinataabika ili kufikia mahitaji yao ya kila siku.