Skip to main content

IOM yaokoa watoto 20 waliokuwa wakisafirishwa kiharamu Ghana

IOM yaokoa watoto 20 waliokuwa wakisafirishwa kiharamu Ghana

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limewaokoa watoto 20 waliokuwa wakisafirishwa kinyume cha sheria kwenye ziwa Volta nchini Ghana uokoaji unaojiri wakati ufadhili wa mradi huo unapofikia kikomo mwaka huu.

Ililazimu Kundi la IOM lililosafiri kwenda kwa vijiji vya Kete-Krachi, Kpando Torkor na Awate-Tornu kushirikiana na utawala wa maneo hayo ili kuokoa baadhi ya watoto.

Watoto 14 waliokolewa mwezi Machi lakini hata hivyo ililazimu IOM kurejea tena juma hili kuwakoa watoto wengine sita ambo pia wangeokolewa wakati huo.