Skip to main content

Pillay akamilisha ziara yake nchini Mauritania

Pillay akamilisha ziara yake nchini Mauritania

Mkuu wa shirika la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa Navi Pillay amekamilisha ziara ya siku mbili nchini Mauritania ambapo alizungumzia changamoto za masuala ya haki binadamu zinazoikabili nchi hiyo na maafisa wa ngazi za juu serikalini pamoja na waakilishi wa mashirika ya umma.

Wakati wa ziara hiyo Pillay alikutana na rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz, waziri mkuu pamoja na spika wa bunge. Pia alifanya mikutano na tume ya haki za binadam,u mashirika yasiyokuwa ya kiserikali , Umoja wa Mataifa na mabalozi . George Njogopa anaripoti

(RIPOTI YA GEROGE)

Wakati wa mkutano wake na maafisa wa serikali nchini humo Bi Pillay amejadilia masuala mbalimbali yakiwemo yale yanayohusu haki za wanawake na pia hakuweka kando hali za mawafungwa na mahabusu.

 

Ametaka kuongezwa kwa kasi ya kuwawezesha wanawake kushiriki kwenye vyombo vya maamuzi, maeneo yanayohusika na utoaji haki na sheria. Amemtolea wito rais wa nchi hiyo kuwaachilia huru wanawake ambao ni wahanga na vitendo vya ubakaji ambao hadi sasa wangali wakisota magerezani.