Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu wazidi kukimbia hali mbaya Somalia:UNHCR

Maelfu wazidi kukimbia hali mbaya Somalia:UNHCR

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeelezea wasiwasi wake kutokana na kuendelea kuzorota kwa hali nchini Somalia suala ambalo limesababisha watu wengi zaidi kukimbia makwao.

Idadi wa Wasomali waliowasili kwenye nchi majirani tangu kuanza mwanzo wa mwaka huu imeongezeka maradufu ikilinganishwa na idadi ya mwaka uliopita. Kati ya mwezi Januari na na Machi mwaka huu karibu wakimbizi 50,000 kutoka Somalia wameandikishwa nchini Kenya , Ethiopia na Yemen.

Kenya ilipokea asilimia kubwa ya wakimbizi hao ambao zaidi ya wakimbizi 31, 400 walioandikishwa nchini Kenya na shirika la UNHCR kwenye kambi ya Daadab wakiwa ni wakimbizi 10,000 kila mwezi anavyoeleza Melisa Fleming kutoka UNHCR.

(SAUTI YA MELISA FLEMING)